MUHAS yagundua dawa za kuongeza kumbukumbu

0
45

Watafiti katika Taasisi ya Tiba ya Asili kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wametengeneza dawa ya kusaidia kuongeza kumbukumbu kwa watu wazima.

Akizungumza katika maonesho ya 46 ya biashara ‘Sabasaba’ jijini Dar es Salaam, Mwanasayansi Mtafiti wa taasisi hiyo, Dk. Benson Mugaka amesema dawa hiyo imepewa jina la ‘Centica capsules’ ambayo imevumbuliwa mwaka huu.

“Kupungua kwa kumbukumbu ni kawaida kwa watu wazima, kwa hivyo tuliamua kutengeneza dawa hii ili kuongeza kumbukumbu zao,” amesema Dk. Mugaka.

Aidha, ameeleza baadhi ya dalili za kuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu kuwa ni pamoja na kusahau mahali ulipoweka kitu baada ya kukitumia kama vile miwani, ufunguo n.k, kusahau majina ya marafiki au kuchanganya kumbukumbu moja na nyingine.

Ametahadharisha kuwa “ingawa ni kweli kwamba mabadiliko fulani ya ubongo hayaepukiki linapokuja suala la kuzeeka, lakini matatizo makubwa ya kumbukumbu si mojawapo. Ndiyo maana ni muhimu kujua tofauti kati ya usahaulifu wa kawaida unaohusiana na umri, na dalili ambazo zinaweza kuonyesha shida ya utambuzi.”

Send this to a friend