Wizara ya Afya imesema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanza huduma ya kuhifadhi mbegu za uzazi ambapo hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema sio lazima watu waende nje ya nchi kufanya upandikizaji, kwani ndani ya hospitali hiyo wanapandikiza na kutunza mbegu hizo kwa kipindi ambacho mtu atakuwa tayari kufanya upandikizaji.
“Mbegu zitahifadhiwa kwa muda wa miaka mitano hadi 10, mtu kama hahitaji mtoto kwa wakati husika zitahifadhiwa, wakati akiona sasa anahitaji kupata mtoto basi atapandikiziwa,” amesema Dkt. Mollel.