
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wamekamatwa kwa kosa la kubandika namba ‘SSH 2530’ kinyume cha sheria.
Kamanda Muliro amesema kuweka namba hizo kwenye vyombo vya moto ni kosa kisheria za usajili kifungu cha sheria namba 13 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya usalama barabarani.
“Tumesisitiza mara kadhaa watu wenye vyombo vya moto wanapoamua kuviingiza barabarani wafuate sheria za barabarani, amesema Kamanda Muliro.
Ameongeza kuwa “Mtu yeyote anayebandika namba hizi, baada ya kufatilia mfumo wa usajili wa namba, hili ni kosa kisheria, na utakuwa unatuhumiwa kuendesha chombo cha moto bila kuwa na usajili ulio rasmi.”








