Mume adaiwa kumuua aliyekuwa mkewe, kisha ajinyonga kisa mali

0
38

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kifo cha Doto Hamisi Magambazi (30) mkazi wa Mjimwema Kiluvya mkoani humo aliyefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu anayedaiwa kuwa mume wake wa zamani, Mbaraka Haruna (42) na kisha kujinyonga.

Jeshi la Polisi limesema Haruna ambaye ni mkazi wa Chanika mkoani Dar es Salaam, alitalakiana na mwanamke huyo mwaka mmoja uliopita, huku chanzo cha mauaji hayo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi na kugombea mali walizochuma pamoja.

Hata hivyo, wakati jeshi hilo likiendelea na msako wa kumkamata mtuhumiwa, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amejinyonga mtini umbali wa mita 300 kutoka nyumbani kwa mwanamke huyo Mtaa wa Mjimwema Kiluvya, kwa kutumia mkanda wa nguo.

Send this to a friend