Mume adaiwa kumuua mkewe na kumzika chumbani

0
15

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamfuatilia mkazi wa Manispaa ya Tabora (ambaye jina lake limehifadhiwa) anayedaiwa kumuua mkewe na kumzika kwenye shimo katika chumba wanacholala chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea Machi 7 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika Mtaa wa Mbilani Kata ya Kidongo Chekundu ambapo baada ya mtuhumiwa kufanya mauaji hayo alimzika chumbani kwao na kisha kusakafia eneo hilo kwa zege.

Ameongeza kuwa mwananchi Michael Hendry ndiye aliyebaini tukio hilo baada ya kuona siku kadhaa zimepita bila chumba hicho kufunguliwa, ndipo waliamua kuvunja mlango wa chumba cha kulala na kukuta chini ya kitanda kuna zege iliyokuwa haijakauka vizuri, na baada ya kuingiwa hofu walifukua sehemu hiyo na kukuta mwili wa Salima Hamisi Maulid (34).

Ajali: Polisi kukagua shule za udereva na namna madereva walivyopata leseni

Aidha, Kamanda Abwao amesema baada ya mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo alikimbia kusikojulikana, hivyo polisi wanaendelea na jitihada za kumtafuta ili kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Chanzo: Habari Leo