Mume ajinyonga ukweni baada ya mkewe kugoma kurudi nyumbani

0
63

Mwanaume mmoja nchini Kenya amejinyonga na kufariki dunia ukweni kwake baada ya jitihada za kumbembeleza mkewe kurudi nyumbani kugonga mwamba.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo ambaye jina lake bado halijafahamika alikwenda ukweni kwake Kijiji cha Kolondo Mashariki mwa Homa Bay, lengo likiwa kumrudisha mke wake aliyekuwa amerudi nyumbani kwa wazazi wake baada ya migogoro ya kifamilia.

Inadaiwa kuwa hapo awali, mwanaume huyo aliondoka na kwenda kusikojulikana, lakini baadaye alirejea usiku kimyakimya nyumbani hapo na kuchukua uamuzi wa kujinyonga.

Daktari: Mtu mmoja anatakiwa kufanya ngono mara tatu kwa wiki

Chifu wa eneo hilo, Perez Okoth amethibitisha kutokea tukio hilo, akisema mwili wa mwanaume huyo ulikutwa ukining’inia kwenye mti ulioko karibu na nyumba ya mama mkwe wake Jumapili, Machi 12 asubuhi.

Kwa mujibu wa maelezo ya wanakijiji tukio hilo siyo la kwanza kutokea, tukio hilo ni la pili kuripotiwa katika nyumba hiyo. Inadaiwa kuwa mwanaume mwingine pia aliwahi kujitoa uhai nyumbani humo katika hali kama hiyo.

Send this to a friend