Mume amkata mke mkono na titi kisa namba ya mwanaume mwingine

0
51

Maria Marwa mkazi wa Kijiji cha Isango wilayani Rorya mkoani Mara amekatwa mkono na Titi na mumewe aliefahamika kwa jina la Werema Ibaso huku akijeruhiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa kichwani.

Tukio hilo lilitokea Septemba 7 mwaka huu majira ya saa tatu usiku, chanzo kikitajwa kuwa wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa mama huyo, baada ya chakula cha usiku mumewe alimuomba simu yake na kumtaka kujaza namba ambazo alikuwa nazo kwenye karatasi ili aone jina lililohifadhiwa katika simu.

Mtoto asafiri zaidi ya 460km kwenye uvungu wa basi

Baada ya kugundua namba hiyo haijahifadhiwa kwenye simu ndipo alipoanzisha ugomvi kwa madai kuwa namba hiyo ni ya mwanaume mwingine ambae amekuwa akiwasiliana nae pasipo yeye kujua.

Inaelezwa baada ya mzozo huo ndipo mwanaume huyo alichukua panga na kuanza kumkata mama huyo kwenye mkono wake wa kushoto na titi lake la kushoto na kisha kumjeruhi maeneo mengine hasa kichwani kisha kukimbia kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi kanda maalum Tarime/Rorya Godfrey Sarakikya amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jitihada za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea na mama huyo kwasasa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara.

Send this to a friend