Mume kizimbani kwa kutishia kumuua mke kisa kupeleka chakula kwa mchungaji

0
42

Joseph Moses dereva wa ‘bodaboda’ mkazi wa Mbeya anayekabiliwa na shtaka la kutishia kumuua mkewe kwa maneno, Irene Mwaikana, ameiambia mahakama kuwa chanzo cha ugomvi huo ni tabia ya mkewe kupeleka chakula kwa mchungaji.

Moses ametoa madai hayo katika Mahakama ya Mwanzo mjini Mbeya chini ya Hakimu Upendo Moshi alipokuwa akitoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Ameiambia mahakama kuwa anafanya kazi kwa shida na kukutana changamoto nyingi hususani ajali za barabarani, lakini pindi anaporudi nyumbani anakuta mkewe amepika chakula na kukipeleka kwa mchungaji.

Serikali kurahisisha gharama za ununuzi wa gesi

“Mheshimiwa Hakimu huyu mwanamke anakera sana, yaani tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio,” amedai.

“Hii tabia imeota mizizi kiasi kwamba nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji mwenyewe hana mke, hivi hata ungekuwa wewe usingehisi vibaya?” amehoji.

Moses anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti Mosi mwaka huu usiku, na ndipo mkewe alipomfikisha mahakamani akidai kutishiwa kuuawa.

Send this to a friend