Museveni akataa kusaini muswada wa mapenzi ya jinsia moja, aurudisha bungeni

0
15

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kutia saini muswada wa sheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja unaotoa adhabu ya kifo katika baadhi ya makosa, akiomba ufanyiwe marekebisho kabla ya kuutia saini kuwa sheria.

Uamuzi wa Museveni ulitangazwa Alhamisi baada ya kikao cha wabunge wa chama tawala ambao karibu wote waliunga mkono muswada ulioidhinishwa na wabunge mwezi uliopita.

Dkt. Mpango: Mapenzi ya jinsia moja, hata wanyama hawafanyi

Taarifa zinasema, wabunge hao wamekubaliana kuurejesha bungeni ili ufanyiwe marekebisho, huku Msemaji wa ofisi ya Rais, Sandor Walusimbi akisema kuwa Rais Museveni hapingani na adhabu zilizopendekezwa katika mUswada huo, bali alitaka wabunge kuangalia suala la urekebishaji wa watu hao.

“[Museveni] aliwaambia wanachama kwamba hana pingamizi na adhabu hizo bali kuhusu suala la urekebishaji wa watu ambao hapo awali walishiriki mapenzi ya jinsia moja lakini wangependa kuishi maisha ya kawaida tena,” ameeleza.

Send this to a friend