Museveni aruhusu Mahakama ya Kijeshi kuhukumu raia

0
2

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesaini marekebisho ya Sheria ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda ((UPDF Amendment Act, 2025), yanayoruhusu raia kuhukumiwa na mahakama za kijeshi katika mazingira maalum.

Serikali imesema sheria hiyo inalenga kuimarisha usalama wa taifa, huku wakosoaji wakisema sheria hiyo inakiuka uamuzi wa Mahakama ya Juu iliyozuia raia kuhukumiwa na jeshi.

Kulingana na sheria hiyo raia yeyote atakayepatikana na silaha kinyume cha sheria atawasilishwa katika mahakama ya kijeshi.

Aidha, serikali ya Uganda imesisitiza kuwa sheria hiyo haitatumika kwa raia wote bali kwa hali maalum tu, ingawa haijatoa ufafanuzi wa moja kwa moja kuhusu vigezo vya hali hizo.