Museveni: Nitashinda kwa asilimia 80 kama hakutakuwa na udanganyifu

0
34

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema anatarajia kushinda kwa asilimia 80 endapo hakutakuwa na udanganyifu wowote katika uchaguzi mkuu unaofanyika leo nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Museveni amesema hana hofu ya kushindwa, akipuuzia uwezekano wa kupoteza uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake, mwanamuziki aliyebadili mwelekeo na kuwa mwanasiasa, Bobi Wine.

Upigaji kura umefanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi. Baadhi ya vituo vya kupigia kura havikufunguliwa kwa wakati kutokana na mashine za uthibitishaji wa wapiga kura kushindwa kufanya kazi. Museveni alisema chanzo cha tatizo hilo kinaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amesema wakati akipiga kura kwamba Waganda wanapaswa kuandamana kwa njia ya amani iwapo uchaguzi utakuwa umefanyiwa udanganyifu.

Send this to a friend