Mustakabali wa bei ya mafuta kujulikana bungeni kesho

0
24

Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta iliyopelekea kupanda kwa bei ya bidhaa, Serikali inatarajia kuwasilisha bungeni mikakati ya dharura itakayowapa unafuu wananchi kujinusuru na janga hilo.

Hii ni baada ya mjadala ulioanzishwa na wabunge waliotaka kufahamu kuhusu mkakati wa Serikali wa kupunguza makali ya bei ya mafuta, huku Mbunge wa Kilindi (CCM), Omary Kigua akitoa hoja ya kuhairishwa kwa bunge ili wabunge wajadili suala la kupanda kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Aidha, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alitoa maagizo kwa Waziri wa Nishati, January Makamba kupeleka bungeni mrejesho Mei 10 mwaka huu kuhusu utatuzi wa jambo hilo.

“Nimewasikia wabunge kuhusu ushauri mlioutoa kwa Serikali juu ya kupanda kwa bei ya mafuta. Hivyo Serikali itafanya nini katika jambo hili, namuagiza Waziri Makamba Jumanne aje na majibu ya namna ya kutatua jambo hili,” Spika wa Bunge.

Send this to a friend