Musukuma ataka wazee wapelekwe JKT

1
44

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Najma Giga ametoa tangazo la fursa ya mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) awamu ya pili mwezi Julai 2022 kwa wabunge vijana ambao hawajawahi kupitia mafunzo hayo.

Hata hivyo, Mbunge wa viti maalum, Ester Bulaya ameomba mafunzo hayo kuwa ya lazima kwa wabunge wote vijana na si hiari ili kuwajengea uzalendo na ukakamavu.

Pia, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ ameomba na wazee washiriki mafunzo hayo kwa kuwa JKT ni sehemu ya kufundisha uzalendo.

“JKT ni sehemu ya kufundisha uzalendo na kwa vile hii taasisi ya Bunge tunahitaji kuwa na uzalendo wa hali ya juu kwanini tunabagua wabunge vijana, kwanini tusiende wote na wabunge wazee,” amehoji Musukuma.

Katika tangazo hilo, limesema mafunzo hayo kwa kawaida yanafanyika katika kikosi cha Jeshi 834 Makutupora, Mkoani Dodoma kwa muda wa siku 38, yakiwa na lengo la kujenga nidhamu, uadilifu, utii, ukakamavu , uvumilivu na uzalendo.

Send this to a friend