Muuguzi aliyeshindwa kumsaidia mjamzito kujifungua asimamishwa kazi

0
68

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Fred Milanzi amemsimamisha kazi muuguzi wa Zahanati ya Basanza, Alex Lyimo ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma za kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.

Hatua hiyo imefuata baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha mama mjamzito (jina limehifadhiwa) akijifungua kwenye zahanati hiyo pasipo msaada wa muuguzi Juni 09,2024.

Milazi amesema pamoja na changamoto iliyojitokeza, mama huyo aliweza kujifungua salama na kupatiwa huduma zote zinazohitajika baada ya kujifungua, kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani Juni 10, mwaka huu.

“Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesikitishwa na tukio hilo na amewaelekeza watumishi wote wa Afya kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia miiko ya taaluma zao na kuwa hatasita kuendelea kuchukua hatua dhidi ya mtumishi yeyote atakayeenda kinyume na miiko na maadili ya utumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu,” ameeleza.

Send this to a friend