Muuguzi Amana afikishwa mahakamani kwa kumbaka, kumlawiti mtoto

0
41

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana jijini Dar es Salaam, Joseph Mwampola (59) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya ubakaji na ulawiti.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Lubonga.

Inadaiwa, mtuhumiwa alitenda makosa hayo katika maeneo mawili tofauti moja ikiwa ni ndani ya hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam ambapo imedaiwa alimbaka binti wa miaka 17 Februari, mwaka huu.

Adaiwa kuua mtoto ili kulipiza kisasi kwa mama yake

Katika shtaka la pili, inadaiwa mtuhumiwa alimbaka binti huyo katika nyumba ya kulala wageni Mei 31, mwaka huu.

Mahakama imeeleza shtaka la tatu linalomkabili mtuhumiwa ni ulawiti, ambapo inadaiwa Februari, 2022 Mwampola alimlawiti binti huyo katika hospitali ya Amana.

Kwa upande wa mshtakiwa alikana mashtaka hayo na mahakama kuahirisha kesi hadi Oktoba 5, 2022 na kwasasa mshtakiwa yuko nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Send this to a friend