Muuguzi Arusha asimamishwa kazi kwa kuigiza kuchoma chanjo ya UVIKO-19

0
42

Wizara ya imeagiza kusimamishwa kazi kwa miezi mitatu Muuguzi Msajiliwa, Scholastica Kanje  anayefanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Arusha, kutokana na kitendo chake cha kufanya mazaha kwenye utoaji chanjo ya UVIKO-19.

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Agness Mtawa amemwagiza Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Arusha mbali na kumsimamisha kazi, atoe taarifa ya zoezi zima lililopelekea muuguzi huyo kufanya kitendo hicho, kwa ajili ya maamuzi zaidi.

Katika video iliyosambaa mitandaoni muuguzi huyo anaonakena akiigiza kumchoma sindano ya chanjo mwananchi, lakini licha ya kuwa hakumchoma, mwananchi huyo alijifanya mithili ya mtu aliyechomwa sindano.

Mtawa amesema kitendo hicho ambacho ni kinyume na sheria na maadili ya uuguzi na ukunga kinaweza kuleta upotoshaji mkubwa na kuzua taharuki kwa wananchi.

Aidha, amewataka wauguzi na wakunga wote kutoa huduma za uhakika kwa wananchi ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Send this to a friend