Muumini alitaka kanisa kumrudishia zaka zake akidai hana mpango tena wa kwenda Mbinguni

0
59

Mwanaume mmoja nchini Nigeria aliyetambulika kwa jina la Chukwudiaso Onyema amelitaka kanisa la Dunamis Church International linalomilikiwa na Mchungaji Dk. Paul Enenche kumrudishia zaka zake alizokuwa akitoa kanisani hapo kwa madai kuwa hahitaji tena kwenda mbinguni.

Onyema amedai amekuwa mwanachama wa kanisa hilo tangu mwaka 2008 na mwanachama hai tangu 2011 ambapo aliambiwa ajiwekee hazina mbinguni kwa njia ya zaka, na sasa hana hamu tena ya kwenda mbinguni hivyo zaka alizotoa kipindi chote ni uwekezaji, na sasa anahitaji fedha zake kutokana na hali mbaya ya kijamii na kiuchumi ya nchi.

Baba aliyembaka binti yake asema alijua ni mkewe

“Kuna shida nyingi nchini Nigeria sasa hivi, njaa na mengine mengi. Nilikuwa nikifanya utafiti katika maktaba yangu na nikagundua kuwa nina uwekezaji katika ufalme wa Mungu. Sipendezwi na ufalme tena, mimi nahitaji tu zaka zangu zote. Tusahau sadaka ninazotoa makanisani, sio tu kwenye vituo vyenu, hata kwenye matawi yenu, sihitaji hilo ninachohitaji ni kile ambacho nina ushahidi nacho. Hizi ni uwekezaji wangu mbinguni,” ameeleza.

Ameongeza kuwa “sitaki hiyo mbingu tena, nimeamua kwenda kuzimu. Mimi sio msumbufu ila nahitaji hizi pesa sasa hivi, nilipumbazwa akili kulipa hela zote, sikuwa na akili enzi zile, lakini sasa hivi nipo na akili zangu, nahitaji hizi pesa na nitashukuru.”

Send this to a friend