Muungano wa Tigo na Zantel utakavyoimarisha huduma za mawasiliano ya simu Tanzania

0
50

Inafahamika kuwa mawasiliano ya simu barani Afrika ni miongoni mwa sekta inayokua kwa kasi zaidi duniani. Ikiwa na mchango mkubwa wa vijana, Afrika inaongoza katika matumizi ya teknolojia ya simu na programu tumishi maarufu kwa Kiingereza kama apps.

Ukuaji wa sekta hiyo unajidhihirisha pia nchini Tanzania. Kwa muda sasa sekta ya mawasiliano nchini humo imekuwa na mchango mkubwa katika ubunifu. Hadi sasa usambaaji wa huduma za mtandao wa intaneti nchini Tanzania umefikia asilimia 40 huku programu mbalimbali za simu kama vile programu za masuala ya fedha kama vile huduma ya fedha kwenye simu imekuwa huduma isiyokwepeka katika maisha yako ya kila siku.

Ukuaji wa sekta hii kwa kiasi fulani umechangiwa na watoa huduma za mawasiliano ambao wamewekeza katika miundombinu ya kisasa na kuweka mtandao ambao unawaunganisha watu nchini kote. Taarifa iliyotolewa mwaka jana kuwa Tigo Tanzania na Zantel zinaungana ilikuwa ni muendelezo wa habari njema kwa sekta hiyo.

Kwa miaka mingi sasa, kampuni hizo mbili zimekuwa zikitoa huduma zenye viwango vya juu kwa wateja wake. Kampuni hizo mbili sasa zipo tayari kuunganisha nguvu ili kutoa huduma bora zaidi visiwani Zanzibar na Tanzania Bara. Mchakato wa kuziunganisha kampuni hizo unaendelea na huenda ukakamilika siku za usoni. Maendeleo haya ni ishara ya hatua chanya kwa wateja wa kampuni zote na sekta hiyo kwa ujumla kwani muunganiko huo utakapomalizika wateja watanufaika kutokana na ongezeko la ubora katika huduma ikiwa ni pamoja na huduma ya fedha na kuimarisha huduma za intaneti.

Vile vile wateja wataona faida ya huduma za mtandao zilizounganishwa na itasaidia kusambaa zaidi kwa upatikanaji wa mtandao wa intaneti kwa wote wanaoishi maeneo ya vijijini.

Send this to a friend