Mvua yasababisha vifo vya watu 12 Dar es Salaam

0
45

Watu 12 wamefariki dunia huku nyumba 107 zikisombwa na maji jijini Dar es salaam kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Oktoba 13 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari na kubainisha kuwa kwa ujumla maeno mengi ya mkoa huo yalikumbwa na athari.

“… athari hizo ni pamoja na vifo vya watu 12… Takribani nyumba 800 zilipata athari za kuzingirwa na maji… na takribani wanachi 480 walikosa mahala pakukaa.”

Kunenge amesema kuwa kati ya waliopoteza maisha, watu 10 ni wanaume na wawili ni wanawake.

Amebainisha kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Mtambani A na B, Mtaa wa Kisutu, Basihaya, Tupendane (Manzeshe), mitaa ya Barafu na kisiwani.

Amesema kwa ujumla maeneo mengi ya jiji hilo yameathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua hiyo.

Send this to a friend