Mvulana afariki akijaribu kuzuia risasi kwa hirizi

0
46

Mvulana aliyejulikana kwa jina la Yusuf Abubakar (12) kutoka nchini Nigeria anadaiwa kuuawa na kaka yake kwa bunduki alipokuwa akijaribu hirizi mpya ya kuzuia risasi.

Polisi katika jimbo la Kwara wanasema wawili hao waliamini kuwa wamejiimarisha kwa hirizi hiyo ya ulinzi ambapo kaka yake alifanya jaribio hilo kwa kumpiga risasi mdogo wake kwa kutumia bunduki ya kizamani inayojulikana kama ‘dane gun’ ambayo inamilikiwa na baba yao.

Mwanafunzi ajinyonga mwalimu kumtaka anyoe nywele

Inasemekana Yusuf alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa risasi, na kaka yake mkubwa kisha kutorokea msituni, huku Polisi wakiendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo.

Licha ya ukosefu wa ushahidi, hirizi hutumiwa na baadhi ya watu nchini Nigeria ambao wanataka ulinzi wanapotenda vitendo vinavyokiuka sheria.

Send this to a friend