Mvulana wa miaka 17 ashikiliwa kwa kuwapa mimba wanawake 10

0
61

Jeshi la Polisi la Jimbo la Rivers Nigeria limemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 17 aliyetambulika kwa jina la Noble Uzuchi na Chigozie Ogbonna (29) kwa madai ya kuwapa ujauzito wanawake 10 kwa ajili ya biashara haramu ya kuuza watoto.

Waliokamatwa wengine ni washukiwa wawili wa kike, Favour Bright (30) na Peace Alikoi (40) ambao wamedaiwa kuendesha kiwanda cha watoto katika maeneo ya Obio/Akpor na Ikwerre katika jimbo hilo.

Imeeleza kuwa Uzuchi na Ogbonna walikodiwa ili kufanya mapenzi na wasichana hao na kuwapa ujauzito.

Mwanafunzi ajiua baada ya kukataliwa na mpenzi wake aliyempa iPhone 14

Msimamizi wa Polisi, Iringe-Koko amesema kwamba uchunguzi uligundua kuwa mwathirika anapojifungua, mtoto walimhifadhi na kumlipa mama kiasi cha N500,000 [TZS milioni 2.5] na kwamba baadhi ya watoto waliojifungua awali walikuwa wameuzwa tayari.

“Waathiriwa wote walikiri kwamba walishawishiwa kwa uuzaji haramu wa watoto kwa sababu ya hitaji la kukabiliana na changamoto za kifedha,” ameeleza

Aidha, Askari wa Kitengo cha Ujasusi  walivamia nyumba mbili, ambapo wahanga wa biashara ya watoto walikuwa wakihifadhiwa na kufanikiwa kuwaokoa wanawake hao.

Send this to a friend