Mwabukusi ashangazwa mahakama kutotoa adhabu ya faini kwa Mchungaji Mwakipesile

0
62

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mbeya imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile kwa kosa la kuendesha kanisa bila ya kuwa na kibali.

Akizungumza na Swahili Times, Wakili Boniphace Mwabukusi amethibitisha kutolewa kwa adhabu hiyo kwa mteja wake akieleza kuwa ni “kweli amehukumiwa lakini mchungaji alikuwa na kibali na taratibu zote alifuata, na alikuwa na rufaa yake inayosubiri usajili wa kanisa lake.”

Aidha, Wakili Mwabukusi ameeleza kuwa sheria inaruhusu kutoa adhabu ya faini na kifungo, hivyo adhabu hiyo ilipaswa ianze kwa kulipa faini na endapo angeshindwa ndipo ahukumiwe kifungo.

Padri aliyetuhumiwa kubaka mtoto wa miaka 12 ashinda kesi

“Kwa kanuni ilitakiwa adhabu ya faini kwanza ianze, akishindwa ndipo afuate kifungo, lakini mahakama siku hizi nadhani ina upungufu wa mahabusu kwahiyo ikaona imfunge badala ya kumpa adhabu,” ameeleza Mwabukusi.

Ameeleza kuwa hatua inayofuata ni kumwombea dhamana mchungaji huyo wakati akisubiri rufaa yake pamoja na kuwasilisha mahakamani hoja zake za rufani.