Mwakinyo agoma kupanda ulingoni, atoa masharti

0
43

Bondia wa nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo ametangaza kutopanda ulingoni Ijumaa Septemba 29, 2023 kupigana dhidi ya bondia Julius Indonga kwa kile alichoita kuwa ni uongo na udanganyifu kutoka kwa mapromota.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwaakinyo ameandika kuwa “… kwetu kama wachezaji wa ndani naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu, wa mapromota.”

Aidha, amesema kuwa “maamuzi ya hili [pambano] kuendelea yako mikononi kwenu [Azam Media], hapa tulipofkia nyinyi binafsi ndio mnaweza kutatua hii changamoto na muda ni leo tu.”

Ramadhani Brothers washika namba 5 America Got Talent

Siku ya Jumatano Septemba 27, 2023 Mwakinyo alibadilishiwa mpinzani ambapo alitakiwa kucheza na Rayton Okwiri wa Kenya ambaye ameripotiwa kuwa amepata majeraha akiwa mazoezini na kutangazwa Indongo kutoka nchini Namibia kama mbadala wake.

Hata hivyo, Mwakinyo hakuridhishwa na mabadiliko hayo katika pambano hilo la kuwania mkanda wa IBA Intercontinental.

Send this to a friend