Mwakinyo akataa wito wa Mahakama, kampuni yataka alipe milioni 150

0
22

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelekeza bondia Hassan Mwakinyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazetini kufuatia kesi ya madai inayomkabili mahakamani hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 13, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi, baada ya Mwakinyo kukataa kupokea hati ya wito wa kufika mahakamani iliyowasilishwa kwake na msambaza nyaraka wa mahakama.

Mwakinyo alifunguliwa kesi ya madai na Kampuni ya PAF Promotion, ambapo pamoja na mambo mengine iliwasilisha madai nane mahakamani hapo, likiwemo la kumtaka bondi huyo kuilipa TZS milioni 150 kampuni hiyo ikiwa ni madhara ya jumla waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni.

Mwakinyo afungiwa mwaka mmoja kwa kukiuka mkataba

Aidha, Shirikisho la Ngumi Tanzania (TPBRC) lilimfungia kwa muda wa mwaka mmoja pamoja na kutozwa faini ya TZS milioni 1 kwa kukiuka mkataba na kushindwa kupanda ulingoni.

Chanzo: Mwanaspoti

Send this to a friend