Mwakinyo alikwenda kushiriki pambano Uingereza bila kibali

0
42

Baada ya bondia wa ngumi za kulipwa nchini , Hassan Mwakinyo kupoteza pambano la kimataifa dhidi ya Liam Smith, imebainika kuwa Mwakinyo alikwenda Uingereza pasipokuwa na kibali cha kucheza.

Akizungumza Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa amedai Mwakinyo alikwenda Uingereza kushiriki pambano hilo bila baraka za Serikali, hivyo kuvunja sheria na kanuni zilizowekwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambazo zilimtaka bondia huyo kupewa vibali ili akacheze pambano.

“Bondia akicheza pambano lolote nje au ndani ya nchi lazima aandike barua kwenda TPBRC, barua hiyo hupelekwa BMT ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa kibali na baraka za kucheza,” amesema.

Serikali: Watanzania wamechoka kuona Taifa Stars ikifungwa kila siku

Palasa amesema Mwakinyo alipofika Uingereza alimpigia simu na kuomba kibali, hivyo hakuwa na budi kumtumia kwa njia ya WhatsApp kwakuwa tayari alishafika nchini na kukamilisha taratibu za kucheza.

Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msitha amebainisha kuwa baraza linakwenda kutekeleza agizo la Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa la kumfuatilia bondia huyo na kutoa mrejesho ndani ya siku 14.

Send this to a friend