Mwakinyo avuliwa Ubingwa wa Afrika

0
43

Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amevuliwa taji la ubingwa wa Afrika (African Boxing Union) kutokana na muda aliotakiwa kuwa ameutetea ubingwa huo kupita.

ABU ilimuondoa Mwakinyo kwenye orodha ya mabingwa na kumshusha hadi nafasi ya tatu ya ubora kwenye uzani wa Super Welter, nafasi ya kwanza ikishikwa na Wale Omotoso kutoka Nigeria, namba mbili ikishikiliwa na Patrick Alotey kutoka Ghana.

Kuvuliwa kwa taji hilo kunakuja ikiwa imepita miezi michache tangu avuliwe taji lingine la ubingwa wa mabara la WBF, hivyo kwa sasa bondia huyo hana taji la ubingwa analoshikilia.

Licha ya masaibu hayo, Mwakinyo anashikilia nafasi ya 14 duniani kwenye uzito wa Super Welter.

Mwakinyo alitwaa ubingwa wa Afrika baada ya kumchapa Bondia kutoka Angola, Maiala Antonio Mei mwaka jana.

Send this to a friend