Mwakinyo: Mapromota waliingia mkataba wa siri na watu tusioelewana

0
14

Bondia maarufu nchini, Hassan Mwakinyo amesema sababu za kutangaza kutoshiriki pambano ni baada ya mapromota kuvunja makubaliano na kuingia mkataba wa siri na watu ambao hawana naye mahusiano mazuri.

Mwakinyo ameyasema hayo kwenye mahojiano ikiwa ni saa chache kabla ya kupanda ulingoni dhidi ya mpinzani wake kutoka Namibia Julius Indonga katika pambano lililopangwa kufanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

“Mwanzoni tulikuwa tukishirikiana katika kila kitu cha maongezi yetu, lakini baada ya kuingia mkataba wa siri, wao wakawa wamenificha mimi kwahiyo nikawa nasikia stori pembeni,” amesema.

Mwakinyo amesema baada ya kugundua mpango huo, aliwataka mapromota kuachana na wafadhili hao kwa sharti la kugharamia malipo ya mkanda alizotaja kugharimu kiasi cha dola 4750 [TZS milioni 11.9] ambazo alizitoa lakini bado waliendelea kushirikiana na watu hao.

Amesema baada ya mkanganyiko ulioendelea, Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa alimtaka kuamua chochote kitakachokuwa sahihi kwakuwa alishushudia sintofahamu zilizokuwa zikiendelea kwa kipindi chote.

Hata hivyo, mapema leo katika mahojiano alisema ikiwa suala hilo litawekwa sawa basi anaweza kuingia ulingoni.

Send this to a friend