Mwalimu akamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi chumbani kwake

0
83

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Nguno, Subiri Andson (37), iliyopo Wilaya ya Itilima, Simiyu, amejikuta katika mkondo wa sheria baada ya kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 7, mwaka huu, ambapo mwalimu huyo alikamatwa na wananchi baada ya kukutwa chumbani kwake na mwanafunzi huyo majira ya saa moja usiku.

Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilayani humo, Jaston Mhule ameieleza mahakama kuwa mwalimu huyo aliwekwa chini ya ulinzi na wananchi wa kijiji cha Nguno kisha kufikishwa katika kituo cha polisi Itilima.

Baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Robert Kaanwa kumsomea maelezo ya kosa hilo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo ambapo upande wa mashtaka uliwasilisha shahidi mmoja na kusikilizwa huku mshtakiwa akipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.