Mwalimu aliyemuua mwalimu mwenzake Geita ajinyonga akiwa chooni

0
45

Mwalimu aliyekuwa akituhumiwa kumuua mwalimu mwenzake kwa kumchoma kisu wakiwa darasani, Samweli Abeli (35) amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia shati lake alipokuwa chooni.

Akitoa taarifa hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Saphia Jongo amesema mwalimu huyo amejinyoonga katika choo cha mahabusu katika kituo kikuu cha polisi Geita, Machi 17, 2023 ambapo alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma ya kumuua Emmanuel Chacha (35), Machi 15 mwaka huu.

“Baada ya mahojiano mtuhumiwa alirudishwa mahabusu, lakini siku ya tarehe 17 majira saa 10 alfajiri mmoja wa mahabusu alienda chooni na kumkuta marehemu Samwel Abel ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya kumuua mwenzie akiwa ananing’inia chooni, alichukua shati lake alilolivaa na kujining’iniza, na mwisho wake akajitundika,” amesema Kamanda.

Mchungaji azikwa baada ya familia kusubiri afufuke kwa siku 600

Ameongeza kuwa mtuhumiwa alichukuliwa na kupelekwa hospitalini baada ya kugundua kuwa alikuwa hajafa na ndipo alipatwa umauti wakati akipatiwa matibabu.

Awali, Kamanda Jongo aliiambia Swahili Times kuwa mtuhumiwa alikiri kufanya mauaji hayo mbele ya wanafunzi darasani huku akidai mwalimu mwenzake ni kikwazo cha maendeleo yake shuleni hapo.

Send this to a friend