Mwalimu bora wa kike ashitakiwa kwa ubakaji wa wanafunzi

0
56

Aliyewahi kuwa mshindi wa tuzo ya mwalimu bora wa mwaka kutoka Texas nchini Marekani amefunguliwa mashtaka ya makosa ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto yanayodaiwa kutokea mwaka 2007.

Brandyn Hargrove (43), mwalimu wa shule ya sekondari Brazosport alikamatwa Desemba 21 na kushtakiwa kwa mashtaka 12 tofauti ikiwa ni pamoja na mashtaka sita ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 15.

Hargrove alikamatwa mwezi Desemba baada ya mwanafunzi huyo wa zamani kufungua mashtaka polisi na kudai kuwa alikuwa katika uhusiano na mwalimu wake wa zamani alipokuwa na umri wa miaka 15 na kwamba unyanyasaji huo ulidumu kwa miaka miwili.

Mahakama yampa ruhusa kukusanya manii ya mume wake aliyefariki

Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa yuko katika miaka yake ya 30, ameiambia polisi kuwa uhusiano huo ulifanyika nje ya eneo la shule.

Taarifa kutoka shule ya Brazosport ambapo Hargrove anafundisha ilisema kuwa mwalimu huyo amesimamishwa kwa muda kutokana na mashtaka hayo, huku mahakama ya nchi hiyo ikimwachilia kwa dhamana.