Mwalimu jela miaka 30 kwa kulawitiwa na mwanafunzi

0
47

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa iliyopo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, aliyetambulika kwa jina moja, Said, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na mwanafunzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema siku za nyuma mwalimu huyo alijenga urafiki na mwanafunzi wa kidato cha nne (19) anayesoma shuleni hapo kwa kumnunulia vitafunwa shuleni hapo.

Amesema baada ya muda, mwalimu alimtaka mwanafunzi huyo akamtembelee nyumbani kwake na ndipo alipoanza kumuonyesha video chafu kupitia simu janja kisha kumsihi amwingilie kinyume na maumbile.

Ameeleza kuwa baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho, ndipo mwalimu alipoanza kumtisha kwa kumwambia asipofanya hivyo atapata adhabu kali mara kwa mara shuleni pamoja na kufukuzwa shule na hapo ndipo alipolazimika kufanya jambo hilo bila ridhaa yake.

Katika hatua nyingine, Bakari Katembe (19), mkulima wa Kijiji cha Mdumbwe amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu.

Katembe alimlaghai mtoto huyo kwa kumununulia pipi kisha kwenda naye nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho.

Send this to a friend