Mwalimu Mkuu anaswa kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi wa darasa la saba

0
40

Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kilimo mkoani Mwanza, Charles Maige amekamatwa kwa tuhuma za kumbaka kwa nyakati tofauti na kumpa ujauzito mwanafunzi aliyekuwa anasoma darasa la saba katika shule hiyo.

Agizo hilo la kukamatwa kwake limetolewa na Mkuu wa Wilaya Misungwi, Poul Chacha baada ya mwalimu mkuu kudaiwa kuwaharibu wanafunzi wa shule hiyo na kuwatishia kuwaua endapo watasema kama anawafanyia ukatili huo.

Mwalimu mwingine aliyetiwa mbaroni ni Venance Komba, anayedaiwa kumshawishi mwanafunzi huyo yatima mwenye ujauzito (jina limehifadhiwa), kushiriki naye kimapenzi, huku akimtisha kufichua siri ya uhusiano wake na mwalimu mkuu wa shule hiyo iwapo hatakubaliana na ushawishi huo.

Mwalimu Mkuu huyo anakabiliwa na tuhuma nyingine za kumtoa mimba mwanafunzi mwingine aliyekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, ili kukwepa mkono wa sheria ikiwa ni pamoja na kuendelea kujihusisha na mahusiano ya namna hiyo na wanafunzi wengine wawili wa darasa la saba.

Kwa mjibu wa mkuu wa Wilaya, inadaiwa kwamba mtoto huyo mwenye umri wa miaka 16 asiyekuwa na wazazi alisitisha masomo kutokana na kupata ujauzito.

Send this to a friend