Mwalimu wa Madrasa adaiwa kulawiti watoto 10 aliokuwa anawafundisha

0
45

Polisi wanamshikilia Mwalimu wa Madrasa anayefahamika kwa jina moja la Faidh kwa tuhuma za kulawiti watoto 10 wa kiume wenye umri kati ya miaka sita hadi tisa waliokuwa wakisoma Madrasa ya msikiti wa Mohamed Shunu ilioko Kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Kamanda wa Polisi  mkoani humo, Janeth Magomi amesema mwalimu huyo wa madrasa alilalamikiwa kufanya tukio hilo Novemba Mosi mwaka huu, saa nane mchana katika Msikiti huo alipokuwa akiwafundisha watoto hao.

Amesema “baada ya kupata taarifa Jeshi liliwafuatilia watoto waliodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo kwa kupata  maelezo yao na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya vipimo ambapo waligundulika kufanyiwa ukatili huo.

Kamanda ameeleza kuwa waliendelea  kumtafuta mtuhumiwa ambaye alitorokea mkoani Kigoma kisha kufanikiwa kumkamata na kumrudisha mkoani Kahama kwa ajili ya kujibu mashitaka yanayomkabili.

Send this to a friend