Mwamuzi wa pambano la Mandonga asimamishwa hadi atakaporudi darasani

0
74

Mwamuzi Habib Mohammed ‘Mkarafuu’ aliyechezesha pambano la Karim Said Mandonga na Salim Abeid amesimamishwa kwa muda baada ya kukiri kushindwa kumudu kuchezesha pambano hilo lililofanyika Septemba 24, 2022 mkoani Mtwara.

Katibu wa Chama cha waamuzi wa ngumi za kulipwa, Emmanuel Mlundwa amesema mwamuzi huyo ametakiwa kurudi darasani kuongeza ujuzi kwenye kozi za waamuzi kabla ya kuruhusiwa kuendelea na majukumu ulingoni.

Amesema Rais wa TPBRC, Chaurembo Palasa hakukosea kufuta matokeo kwa kuwa kama yangeingizwa kwenye rekodi, mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec) ungehitaji video zake kwanza.

“Kama Chama tumejiridhisha kuwa kulikuwa na makosa mengi ya kiuamuzi kwenye pambano hilo, huenda yamechangiwa na waamuzi wetu kukaa muda mrefu bila kushiriki kwenye kozi mbalimbali na ndicho kimetokea kwa Mkarafuu,” amesema Mlundwa.

Matokeo ya pambano hilo yalifutwa baada ya mwamuzi kuonyesha kutolimudu ambapo Mandonga alipigwa na kudondoka chini lakini hakumhesabia kama kanuni zinavyotaka hadi aliponyanyuka.

Send this to a friend