Mwanachuo ashikiliwa kwa mauaji ya mwenzake kisa ulevi

0
2

Polisi mkoani Mbeya wanamshikilia Emilian Duzu (21) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi mwenzake wa chuo hicho, Gerald Said (22).

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa Juni 14, 2025 saa 11 alfajiri, katika klabu ya Mbeya Pazuri iliyopo jijini Mbeya, mtuhumiwa Emilian anadaiwa kumchoma Gerald na kitu chenye ncha kali tumboni hali iliyopelekea kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu, lakini ilipofika saa 7 mchana alifariki.

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokana na ulevi wa kupindukia wakiwa ndani ya klabu hiyo ambapo walinzi waliwaamua na ndipo mtuhumiwa alitoka nje na kuelekea eneo la maegesho alipokuwa ameegesha gari, kisha Gerald alimfuata kwa lengo la kuendelea kugombana, ndipo mtuhumiwa alimchoma kwa kitu chenye ncha kali,” imeeleza taarifa.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa baadhi ya wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani havina nafasi katika jamii, na kwamba halitasita kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Send this to a friend