Mwanafunzi ajifungua katika chumba cha mtihani

0
48

Mwanafunzi wa darasa la saba katika  Shule ya Msingi Kulimi, Kata ya Kulimi wilayani Maswa, mkoa wa Simiyu amejifungua katika chumba cha mtihani Julai 27, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na ofisa elimu mkoa huo, Majuto Njaga katika mahojiano na Mwananchi imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 27, mwaka huu wakati mwanafunzi huyo akiwa katika chumba cha mtihani.

Wazazi wawaogesha watoto kwa dawa za mvuto wa mapenzi ili waolewe

Amesema idara ya elimu wilayani Maswa ilitoa taarifa katika ofisi yake na kueleza kuwa walimu hawakuwa wanafahamu kama mwanafunzi huyo ni mjamzito katika kipindi chote cha ujauzito wake.

“Alijifungua akiwa shuleni, baada ya kujifungua, ofisi ya elimu kwa kushirikiana na maafisa wa ustawi wa jamii walifika shuleni hapo na binti alimtaja aliyempa ujauzito na tayari kesi imefunguliwa,” amesema.

Majuto amesema baada ya maafisa wa ustawi wa jamii kufika shuleni alikabidhiwa kwa wazazi wake akiwa na mwanaye kwa ajili ya uangalizi zaidi na ataruhusiwa kurudi shuleni baada ya mwaka mmoja kwa mujibu wa waraka wa elimu uliopo.

Chanzo: Mwananchi.

Send this to a friend