Mwanafunzi ajiua baada ya kukataliwa na mpenzi wake aliyempa iPhone 14
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Gunze Luhangija aliyekuwa akisomea Shahada ya Menejimenti ya Ushirika na Uhasibu (BCMA), amekutwa amejinyonga chanzo kikisemekana ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na kukataliwa na mpenzi wake.
Inadaiwa alishawahi kujaribu kujiua kwa kunywa sumu Januari 4 mwaka huu lakini aliokolewa baada ya kukataliwa ilihali ikieleza kuwa alimgharamikia mpenzi wake huyo ikiwemo kumpangishia nyumba.
Raia wa Kenya adukua mifumo ya Zimbabwe na kuiba bilioni 280
Baadhi ya wanafunzi kutoka chuoni hapo wamedai marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake siku chache baada ya kumnunulia simu janja aina ya iPhone 14 iliyopelekea kuwa katika hali ya msongo wa mawazo.
“Siku ya Boxing Day alimnunulia mpenzi wake iPhone 14 na baada ya siku chache demu (mpenzi) alimkataa kwamba kapata mtu mwingine [..] dogo kajitundika,” mmoja wa wanafunzi chuoni hapo.
Aidha, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Yahya Mdogo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake.