Mwanafunzi ajiua baada ya kuliwa ada ya chuo kwenye kamari

0
35

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Federal Polytechnic, Ilaro (FPI) nchini Nigeria amejiua baada ya kutumia ada yake ya chuo na ya mwanafunzi mwenzake kucheza kamari mtandaoni na kushindwa.

Kulingana na Shirika la Habari la Nigeria (NAN), Samuel Adegoke, mwanafunzi wa Diploma ya Uhandisi wa Umeme, aliripotiwa kunywa sumu siku ya Jumatatu wakati wenzake walipokuwa wakijiandaa na mtihani wa muhula wa kwanza baada ya chuo kuonya kuwa hakuna mwanafunzi atakayesajiliwa kufanya mtihani bila kukamilisha ada.

Inaelezwa kuwa baada ya kupoteza pesa zake katika kamari mtandaoni siku ya Ijumaa, Adegoke alidaiwa kuiba pesa za mwenzake kwa kupata nywila yake (password), lakini pia akapoteza.

Biharamulo: Walimu 6 watuhumiwa kujihusisha na biashara ya kuwauza wanafunzi kingono

Naibu Msajili wa FPI, Sola Abiala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa chuo kilimpeleka mwanafunzi huyo katika hospitali ya maalum ya Hossanah, lakini alifariki muda mfupi baada ya kulazwa.

Ameongeza kuwa baba yake Adegoke amekataa kuuchukua mwili wa kijana wake, huku akiuambia uongozi kwamba awali mtoto wake alipoteza ada pia kwa kucheza kamari, lakini yeye (baba yake) alitatua tatizo kwa kufanya malipo mengine.

“Tulipomwomba baba achukue mwili huo, alikataa akisema hawezi kuupeleka mwili wa mtoto wake nyumbani. Alituomba tumzike,” amesema Abiala.

Send this to a friend