Mwanafunzi aliyeandika barua ya kuacha shule apata ufadhili wa masomo

0
50

Taufiq Hamis (15), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbati ambaye hivi karibuni alizua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumuandikia barua mkuu wa shule akitoa azma yake ya kuacha shule ili akafanye shughuli za uvuvi kwa ajili ya kuisaidia familia, amepata udhamini wa masomo katika Shule ya Sekondari Ocean.

Mwanafunzi huyo pamoja na mwenzake Issa Abdallah (15) ambaye pia alichaguliwa katika shule ya Sekondari Mbekenyela na kuacha masomo yake na kufanya shughuli za madini ili kuisaidia familia yake wamefanikiwa kupata udhamini huo katika shule hiyo iliyoko Mikindani mkoani Mtwara .

Meneja wa Shule ya Ocean, Juma Nchia ameeleza kuwa taasisi mbili za kalamu Education Foundation (KEF) pamoja na Mar’wa Education Centre inayomiliki shule ya Ocean kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali, wameamua kuwachukua wanafunzi hao na kuwahamishia katika shule ya Sekondari ya Ocean iliyopo mkoani hapo.

Taufiq amewashukuru wahisani hao na kusema kuwa, sasa ndoto zake za kuwa rubani wa ndege zitatimia, huku mwanafunzi Issa akisema kuwa aliachana na shughuli za madini baada ya mmoja wa walimu kumuona na kumshauri kurudi shuleni na hatimaye kupata udhamini.

Send this to a friend