Mwanafunzi ampiga mwalimu hadi kupoteza fahamu

0
43

Polisi nchini Nigeria wanamshikilia mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Ilorin kwa tuhuma za kumpiga mhadhiri wa kike.

Taarifa ya polisi inaeleza kuwa mwanafuzi alikwenda kumwona mhadhiri huyo kuhusu tasnifu yake ya mwaka wa mwisho, ndipo mvutano baina yao ukaibuka.

Mwanafunzi huyo anatuhumiwa kumshambulia mhadhiri wake na kumjeruhi kichwani hadi kupoteza fahamu.

Mhadhiri huyo anaendelea na matibabu na
mwanafunzi amewekwa chini ya ulinzi wa polisi.

Msemaji wa chuo, Kunle Akogun amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika taarifa rasmi, na kusisitiza kuwa mhadhiri anaendelea vizuri.

Send this to a friend