Mwanafunzi ashikiliwa kwa kuchoma moto madarasa

0
38

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Yesse Charles (17), mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Lyela, kwa tuhuma za kuchoma vyumba viwili vya madarasa ya shule hiyo Septemba 13, mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema mwanafunzi huyo alitumia mabua na karatasi kuwasha moto katika vyumba hivyo ambapo kimoja kilikuwa kikitumika kama bweni na kusababisha uharibifu wa mali ikiwepo vifaa vya wanafunzi wa kidato cha nne ambao walikuwa wakijiandaa na mitihani.

“Vyumba viwili viliteketea kwa moto lakini kimoja kati ya hicho kimekuwa kikitumika na wanafunzi wa kidato cha nne kama bweni kwa ajili ya kujiandaa na mtihani, hivyo moto huo umesababisha vitu mbalimbali kuteketea,” amesema kuzaga.

Kenya: Erick Omondi ahukumiwa kifungo jela

Aidha, Kamanda amesema uchunguzi umebaini chanzo cha tukio hilo ni chuki za mtuhumiwa baada ya kuadhibiwa na mwalimu kutokana na tabia yake ya utovu wa nidhamu ambao ulimfanya kutohudhuria vipindi darasani.

Send this to a friend