Mwanafunzi atolewa korodani baada ya kupigwa na walimu wake

0
41

Polisi katika Kaunti ya Kisii nchini Kenya wanawasaka walimu wa Shule ya Sekondari ya Nyabisia huko Bobasi kutokana na adhabu kali ya viboko iliyotolewa kwa mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 19 kwa madai ya kuvunja sheria za mitihani.

Mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa amelazwa hospitalini baada ya korodani yake moja kutolewa na madaktari, amesimulia kuwa wakati mitihani ikiendelea shuleni, wanafunzi walipata moja ya karatasi iliyovuja iliyokuwa ikisambazwa kabla ya mmoja wa walimu kumkamata akiwa na wanafunzi wengine.

Baba atuhumiwa kumlawiti mtoto wake wa mwaka mmoja

Ameongeza kuwa walimu watano akiwemo mwalimu wake wa hesabu na mlinzi wa shule hiyo walimshambulia kwa mateke na makofi kisha kupelekwa kwenye darasa lililotajwa kuwa ‘chumba cha mateso’ cha shule hiyo ambapo alifungwa kwenye gogo huku miguu yote miwili ikiwa imetenganishwa na kumpa kipigo kikali.

Mwanafuzi huyo amedai aliwasihi waalimu kufuta mtihani wake ili kumuachia, lakini waalimu hao hawakusikiliza ombi lake na kisha walipogundua madhara yaliyotokea, walimwambia asiripoti jambo hilo kwa mkuu wa shule.

Madaktari wamesema moja ya korodani ilibidi iondolewe kwani ilikuwa imeathiriwa vibaya kutokana na kupigwa sana.

Send this to a friend