Mwanafunzi ajiteka mwenyewe ili kupata fedha kwa wazazi

0
39

Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanafunzi wa ya Udaktari, Edwin Kamau (23), ambaye anadaiwa kuwa ametekwa kwa nia ya kujipatia pesa kutoka kwa wazazi wake.

Mwanafunzi huyo kutoka Chuo cha Mafunzo ya Udaktari cha Makindu anasemekana kujificha Jumapili iliyopita na kumpigia simu mama yake akidai kutekwa nyara.

Kamua alimwambia mama yake kwamba watekaji nyara walitaka fidia ya Ksh.70,000 (sawa na TZS milioni 1.38) ili kumwachilia huru kabla ya kumnyonga.

“Wazazi wake waliokuwa wamechanganyikiwa waliripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi ambao mara moja walianzisha msako wa kuwatafuta watekaji nyara. Hata hivyo, simu hizo ziliendelea kupigwa huku Kamau akimwambia mama yake kwamba watekaji nyara walikuwa wakikaribia kummaliza,” mamlaka nchini humo imeeleza.

Aidha, katika juhudi za kuokoa maisha ya mtoto wao, wazazi hao walituma awamu ya kwanza ya Ksh.10,000 (TZS 197,543)Julai 6 ambayo aliitumia kwa kujifurahisha yeye mwenyewe pamoja na mwanamke aliyekutana naye katika sehemu ya starehe.

Kulingana na Mamlaka ya Upelelezi ya Jinai (DCI) mwanamke huyo alimuwekea kitu kisichojulikana katika kinywaji chake na kupoteza fahamu kisha kumuibia pesa zake.

Baada ya Kamau kupata fahamu, siku ya Alhamisi aliwapigia simu wazazi wake akidai kuwa watekaji wake walikuwa wakidai pesa, kisha wakamtumia tena kiasi cha Ksh. 40,000 (TZS 790,000).

Hata hivyo, Maafisa wa upelelezi waliokuwa wakifuatilia suala hilo walimkamata na kumkuta na Ksh. 38,600 (TZS 762,517), walipomhoji alidai alikuwa akijaribu kurejesha karo ya shule ya muhula uliopita ambayo aliifuja

Send this to a friend