Mwanafunzi Esther aliyepotea shuleni apatikana

0
84

Mwanafunzi wa Sekondari ya Panda Hill iliyoko mkoani Mbeya, Ester Noah Mwanyilu aliyepotea Mei 18, mwaka huu amepatikana katika eneo la Ifisi, mkoani humo.

Kwa mujibu wa Clouds Media, mwanafunzi huyo yuko kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano ili akabidhiwe kwa familia yake.

Polisi wawasaka wazazi wa mwanafunzi aliyeolewa

Juni 22 mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa alitoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Kamati ya Usalama ya Mkoa huo kutafutwa kwa mwanafunzi huyo baada ya kupokea ‘clip’ yenye maelezo ya mzazi wa binti huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha tano, tahsusi ya PCB.

Esther aliacha ujumbe wa maandishi akiwaaga rafiki zake na kuomba mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfayia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu.

Send this to a friend