Mwanafunzi Esther: Nilitoroka shuleni kwa sababu mwalimu alinibaka

0
48

Mwanafunzi kidato cha tano wa Shule ya Sekondari Panda hill, Esther Noah (18) amesema chanzo cha kutoroka shuleni ni kunyanyaswa kingono na mwalimu wa shule hiyo anayejulikana kwa jina la mwalimu Jimmy.

Akizungumza na Habari Digital, Esther amedai mwalimu huyo alikuwa akimtaka kimapenzi na baada ya kumkatalia ndipo alianza kumnyanyasa kwa vipigo, na kisha kumbaka bwenini huku akimziba kwa blanketi ili asitoe sauti za kuomba msaada.

“Tulipotoka kuchukua chakula tukawa tumefika bwenini kwa kuchelewa, tukala chakula kisha mimi nikaenda kuoga, wakati narudi bwenini walimu wakawa wamefukuza watu maana muda ulikuwa umekwisha. Nilipofika mimi nikawa napaka mafuta, ndipo mwalimu [Jimmy] akaingia akawa ananipiga nikamwambia nimechelewa kuchukua chakula, na ndipo akanibaka,” ameeleza.

Ameongeza kuwa kesho yake baada ya kutendewa tukio la ubakaji, wakati wakiendelea na mitihani alizushiwa kuwa ameingia na kitabu kwenye chumba cha mtihani ambacho kilikuwa chini ya dawati lake, na kisha akashambuliwa kwa kipigo na walimu na kuchaniwa mtihani licha ya kujitetea kuwa hakuhusika.

“Ilibidi niende zahanati [ya shule] na baada ya mtihani wa pili kuisha nikaenda kushinda kanisani, nilikuwa nalia sana kwamba kwanini nimetendewa kitendo kile jana yake na leo nasingiziwa? Nikaamua kutoroka shuleni. Niliandika barua nikiwa na hisia kali na maumivu na kwenda kusikojulikana,” amesema.

Amwagiwa tindikali akidai kugawana mali na mumewe

Aidha, kuhusu kijana muuza mkaa aliyejulikana kwa jina la ‘Baba Jose’ ambaye alimtambulisha kama mke wake kwa mwanamke ambaye Esther alikutwa akiishi nyumbani kwake, mwanafunzi huyo amedai kijana huyo alimpeleka kwa mwanamke huyo ili kumsaidia apate kazi, na baada ya hapo hawakuwahi kuonana tena.

Esther pamoja na familia yake wameiomba Serikali kumchukulia hatua mwalimu huyo ili vitendo vya unyanyasaji na ubakaji unaofanywa na baadhi ya walimu vikomeshwe.

Send this to a friend