Mwanafunzi UDOM ajirusha ghorofani akidai amefelishwa makusudi

0
64

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Shule ya Uuguzi na Afya ya umma (SoNPH), Ezekiel Sostenes amelazwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati, Benjamin Mkapa baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne.

Kabla ya tukio hilo lililotokea Desemba hapo jana 15, 2022 kulikuwa na ujumbe wa WhatsApp ambao ulisambaa mitandaoni ukionesha majibizano kati ya mwanafunzi huyo akimlalamikia mkufunzi wake kuwa alimfelisha kwa makusudi.

Akizungumza na Mwananchi Dkt. Winnie Msangi kutoka hospitalini hapo amesema walimpokea mwanafunzi huyo jana akiwa kwenye hali mbaya.

Dkt. Winnie amesema mwanafunzi huyo anaendelea na matibabu baada ya kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo ofisa habari wa Chuo cha UDOM, Beatrice Mtenga amesema kuwa hana taarifa za tukio hilo na kuomba kupewa muda wa kulifuatilia.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend