Mwanafunzi wa kike atoweka Mbeya, aacha ujumbe kumhusu Mwalimu

0
48

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameamuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Kamati ya Usalama ya Mkoa huo wafanye uchunguzi zaidi na kwa haraka kuhusiana na tukio la kupotea kwa mwanafunzi, Esther Mwanyiru anayesoma shule ya Sekondari Panda Hill mkoani humo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Juni 22, 2023 baada ya kupokea kipande cha video chenye maelezo ya mzazi wa binti huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha Tano, tahsusi ya PCB kwenye shule hiyo.

Katika kiande hicho, mama yake Esther anadai yeye na mume wake waliitwa na uongozi wa shule hiyo na kujulishwa kwamba Esther hajaonekana tangu asubuhi ya tarehe 18 Mei, 2023 na kwamba hadi sasa zimepita siku zaidi ya 20 na wamekuwa wakimtafuta binti yao kila mahali lakini hakuna dalili za kumpata.

Polisi wawasaka wazazi wa mwanafunzi aliyeolewa

Amedai kuwa Esther aliacha ujumbe wa maandishi akiwaaga rafiki zake na kuomba mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfayia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu.

“Naomba umfikishie salamu Mwalimu Jimmy, mwambie ameyafanya maisha yangu kuwa magumu sana hapa shuleni. Asiendelee kuwafanyia wanafunzi wengine kama alivyoyafanya maisha yangu mimi kuwa magumu,” amesema mama yake Esther wakati akisoma sehemu ya ujumbe huo.

Send this to a friend