Mwanafunzi wa miaka 16 apewa ujauzito na mzee wa miaka 65

0
42

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamtafuta Amos Samson (65) mkazi wa Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 16.

Mwanafunzi huyo amedai amepewa ujauzito na mzee huyo baada ya kumshawishi kwa kumpa shilingi 2,000 na kumwingilia kimiwili, kisha kupewa tena shilingi 5,000 alipomuita nyumbani kwake na kufanya nae kitendo hicho.

Ameongeza kuwa aliendelea kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mzee huyo tangu Desemba 2022 mpaka alipobainika kuwa na ujauzito unaokadiriwa kuwa na miezi mitano.

Mwalimu mkuu anaswa kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi wa darasa la saba

Amedai mahusiano yao yalibainika baada ya mzee huyo kumtaka kimapenzi ndugu yake jambo ambalo alichukizwa nalo na kuamua kufichua siri hiyo.

Akizungumza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi amesema polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo anayedaiwa kutoroka huku Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akithibitisha kuwa binti huyo ni mjamzito wa miezi mitano .

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend