Mwanaharakati wa Kenya Bonface Mwangi aondolewa mashitaka ya ugaidi

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) nchini Kenya imemwondolea mashitaka ya ugaidi mwanaharakati Boniface Mwangi, ambaye sasa atakabiliwa na mashtaka ya kumiliki risas bila kuwa na cheti halali cha kumiliki silaha.
Awali, alishtakiwa kwa kusaidia shughuli za kigaidi zinazohusishwa na maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika Juni 25, 2025.
Kukamatwa kwake kuliibua taharuki na mjadala mkubwa mitandaoni, huku mamlaka zikidai kuwa zilikuta vitu vilivyotajwa kuwa na hatari kwa usalama wa taifa.
Hata hivyo mahakama imemwachia kwa dhamana ya Sh milioni 1 [TZS milioni 20].







