Mwanamke (56) adaiwa kumbaka mtoto (8), amchubua sehemu za siri

1
17

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Desderia Mbelwa (56) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Iringa kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema tukio hilo limetokea Mei 8 katika Kijiji Cha Lumuli, Wilaya ya Iringa Vijijini ambapo mtuhumiwa alimkamata kwa nguvu mtoto huyo kisha kumbaka na kumsababishia michubuko na maumivu makali sehemu zake za siri.

Arusha: Mmiliki wa madrasa adaiwa kulawiti wanafunzi 22

“Alimkamata kwa nguvu mtoto huyo anayesoma darasa la tatu alipokuwa anatoka shule na kumvutia kichakani. Baada ya kumvutia kichakani alimtishia asiseme na kufanya naye ngono, kitendo kilichomsababishia mtoto huyo  maumivu makali na majeraha katika sehemu zake za  siri,” amesema Kamanda Bukumbi.

Aidha, ameongeza kuwa mtuhumiwa amekiri kufanya kitendo hicho bila kutaja sababu za kufanya hivyo, na kuwa amesema baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Send this to a friend